KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 7, 2013

Daniel Sturridge nje kikosi cha England kitakacho vaana na Ukraine.

Mshambuliajiwa wa Liverpool Daniel Sturridge ameondolewa katika kikosi cha England kitakacho kabiliana na Ukraine ukiwa ni mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga fainali ya kombe  la dunia kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya msuli wa paja.

Sturridge mwenye umri wa miaka 24, amerejea katika klabu yake kwa ajili ya matibabu kabla ya mchezo wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Moldova hapo jana na ameshindwa kuponya maumivu yake ya nyama za paja kabla ya kuelekea mjini Kiev kuvaana na Ukraine siku ya Jumanne.

Majeraha ya wachezaji wengine akiwemo Wayne Rooney na Andy Carroll, pamoja na kusimamishwa kwa Danny Wellbeck kunamfanya meneja Roy Hodgson kukosa chaguo mbadala kueleka katika mchezo huo.
Hakuna mchezaji mbadala aliyeitwa mpaka sasa.