Steven Gerrard anasema inabidi waaminiwe wakati wakielekea kucheza mchezo mwingine muhimu wa kusaka nafasi ya kutinga fainali ya kombe la dunia Jumanne dhidi ya Ukraine.
England kwasasa inaongoza kundi H ikiwa na alama 15 baada ya ushindi wao wa jana wa mabao 4-0 dhidi ya Moldova ikiwa sasa inalingana kwa alama na Montenegro lakini wakiwa juu kutoka na uwiano mkubwa wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ukraine iko nyuma kwa alama moja kutoka kwa vinara hao wa kundi ikiwa katika nafasi ya tatu.
Lakini hata hivyo nahodha huyo wa England amenukuliwa akisema "We have nothing to fear and can go there full of confidence."
World Cup Qualifying Group H
|
Played | Won | Points |
---|---|---|---|
England |
7 |
4 |
15 |
Montenegro |
8 |
4 |
15 |
Ukraine |
7 |
4 |
14 |
Poland |
7 |
2 |
10 |
Moldova |
8 |
1 |
5 |
San Marino |
7 |
0 |
0 |
Wakati kikosi cha Roy Hodgson kikiwashinda Moldova katika uwanja wa Wembley, Ukraine waliwashindilia San Marino kwa mabao 9-0.
Rickie Lambert anatarajiwa kuongoza safu ya ushanbuliaji ya England Jumanne huku Wayne Rooney akiwa majeruhi na Danny Welbeck akiwa anatumikia adhabu ya kusimama kwa mchezo mmoja.
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, ambaye amekosa mchezo wa Moldova anaendelea kuwa katika wasiwasi kutokana kukabiliwa na majeraha
England's remaining qualifiers
10 September: a v Ukraine11 October: h v Montenegro
15 October: h Poland
No comments:
Post a Comment