Ilori anakuwa usajili mpya wa sita wa Liverpool.
Sakho akionyesha jezi yake.
Ilori akipozi ndani ya viunga vya uwanja wa mazoezi wa Melwood.
Ilori played at Anfield in the 2011/2012 Next Gen Series
Liverpool imethibitisha kuwasajili walinzi Tiago Ilori kutoka katika klabu ya Sporting Lisbon na Mamadou Sakho kutoka katika klabu ya Paris Saint-Germain.
Wachezaji wote hao walikuwepo jukwaani katika mchezo wa Jumapili wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United katika eneo wanalokaa wakurugenzi wa timu na wamekamilisha mpango wao wa uhamisho baada ya kufanikiwa katika vipimo vya afya vilivyo fanyika uwanja wa mazoezi wa Melwood.
Ilori, ambaye alizaliwa mjini London, amekuwa akiiwakilisha Ureno katika timu zake za taifa za chini ya miaka U18, U19 na U20.
Ilori na Sakho wanakuwa wachezaji wa sita na saba kusajiliwa naq meneja Brendan Rodgers katika kipindi cha usajili wa kiangazi wakifuata nyayo za Kolo
Toure, Iago Aspas, Luis Alberto, Simon Mignolet na Aly Cissokho.
FA inataka kufanya mazungumzo na Liverpool juu ya mlinzi huyo ambaye inadhaniwa kuwa anaweza kuwa anaruhusiwa kuichezea England kimataifa.
Ilori wakati akiitumikia Sporting Lisbon dhidi ya Benfica.
Ilori (katikati) akiwa karibu na Sakho (kushoto) na mchezaji mwingine mpyaVictor Moses (kulia) ndani ya Anfield Jumapili
Sakho akiwa ndani ya Ufaransa na klabu yake ya PSG.
No comments:
Post a Comment