Licha ya kusajiliwa na kuwa mchezaji ghali kuliko wote duniani, Gareth Bale anasema Cristiano Ronaldo ndiye bosi ndani ya Real Madrid.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ametambuliashwa mchana wa leo ndani ya uwanja wa Bernabeu kwa uhamisho wa rekodi ya dunia wa pauni milioni £86 akitokea katika klabu ya Tottenham.
Lakini licha ya kuhama kwa uhamisho wa juu zaidi (astronomical fee), kwake aliichukulia tukio la kukamilika kwa usajili wake kama neema kuwa galactico.
'Cristiano kwangu ni bora duniani na hiyo ndiyo sababu ya mimi kuamua kuja hapa'.
'Sidhani kama nahitaji kumsaidi Cristiano kuwa mchezaji bora duniani kwani ameshakuwa tayari.
'Cristiano ni bosi hapa ni mchezaji bora duniani. nataka kujifunza kutoka kwake'
No comments:
Post a Comment