Kocha wa zamani wa Manchester City ,Roberto Mancini
anazungumza na mabingwa wa Uturuki Galatasaray kuhusu nafasi iliyo wazi
ya kocha wa klabu hiyo.
Klabu hiyo ya mjini Istanbul imethibitisha
katika mtandao wa Twitter kwamba Mancini amekutana na wakurugenzi wa
klabu hiyo na kupigwa picha na mkurugenzi mkuu , Lutfi Aribogan.
Mtaliana huyo anatarajiwa kushika
nafasi ya Fatih Terim, ambae alipigwa kalamu wiki iliyopita baada ya
kushindwa kukubaliana mkataba mpya.
Manchester City ilimfuta Mancini mnamo mwezi wa Mei mwaka mmoja baada ya kuongoza hadi kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Galatasaray imeanza vibaya msimu wa soka Uturuki ikishinda mechi moja tu kati ya michuano mitano ya kwanza .
Katika michuano ya klabu bingwa ya Ulaya ilicharazwa na Real Madrid,kwa mabao 6-1.
Terim, mwenye umri wa miaka 60, aliongoza
Galatasary kushinda mara 6 ubingwa wa Uturuki pamoja na kombe la UEFA
mwaka 2000 baada ya kuichezea kwa kipindi cha miaka 11.
Mancini ameshinda ubingwa wa Italia mara tatu
akiwa na Inter Milan ya Utaliana kabla ya kunyakua kombe la FA na
ubingwa wa ligi na Manchester City.
No comments:
Post a Comment