Kitongoji cha Soweto Afrika kusini. |
Ugomvi umeibuka baina ya watayarishaji wa mbio za
Soweto Marathon wakisema mbio hizo hazitofanyika tarehe 3 Novemba wakati ambapo James Evans Rais wa shirikisho la riadha Afrika Kusini akisema mbio hizo
zitaendelea kama ilivyopangwa.
Vijana wa Soweto Marathon Trust walioanzisha
mbio hizo wamesema kuwa kuna wasiwasi kuwa bwana James Enas huenda
akazipeleka mbio hizo mjini Cape Town anakotokea lakini kamwe
hazitofanyika eneo la Soweto.
Wanamlaumu James Evans kwa kutumia
pesa za kuandaa mbio hizo kwa mambo mengine na pia Bwana Evans hataki
kusema kiasi gani wafadhili walichotoa.
Hata hivyo James Evans anasema kuwa baadhi ya
ripoti zinazosema kuwa mbio hizo zimefutiliwa mbali na Soweto Marathon
trust ni sehemu njama ya kutaka kumng'oa madarakani.
Mfuko huo wa Soweto Marathon Trust unahitaji
dola mia 5 elfu kuandaa mashindano hayo yaliyoanzishwa mwaka 1991 yakiwa
maarufu kupita yote barani Afrika.
Mshindi wa mbio hizo mwaka jana alikua Shadrack
Kemboi wa Kenya. Sasa Soweto Marathon Trust wanamtaka waziri wa Michezo
wa Afrika Kusini Fikile Mbalula (Vuvuzela ) aingilie kati.
No comments:
Post a Comment