Nyota wa Barcelona Lionel Messi na babake wamefika katika mahakama moja ya Uhispania kujibu mashitaka yanayohusiana na kesi ya kukwepa kulipa kodi ya mamilioni ya euro.
Messi alitoa majibu kwa takribani nusu saa baada ya babake Jorge Horacio Messi kuulizwa maswali. Baada ya wote wawili kuondoka mtu na njia yake, wakili wa Messi alizungumza nje ya chumba cha mahakama hiyo ya mjini Gava, kusini mwa Barcelona, karibu na makaazi ya Messi. Wakili wa mshambuliaji huyo amesema familia ya Messi ilitaka kuonyesha uwazi, na hali ya ushirikiano na sasa mambo yamekwenda sawa.
Kama atapatikana na hatia Messi na babake wanaweza kutozwa faini ya hadi
asilimia 150 ya kiasi cha fedha wanachodaiwa kama deni. Inadaiwa
walipata faida kubwa na wakakwepa kulipa kodi kwa kutumia makampuni ya
ng'ambo kama vile Uruguay. Wote wawili wanakanusha madai hayo na hata
kuungwa mkono na rais wa Barcelona Sandro Rosell na rais wa zamani Joan
Laporta.
Babake Messi alifanya malipo ya zaidi ya euro milioni 5 mnamo Agosti 14
kugharamia madai hayo ya madeni ya kodi na riba. Malipo hayo yaliifanya
mahakama kuamua kuwa Messi na babake hawakustahili kuwasilisha ombi la
dhamana. kesi hiyo hata hivyo haijamzuia Messi dhidi ya kufanya kazi
yake. Kwa sasa anaongoza katika ufungaji wa mabao mengi katika Laliga
akiwa na mabao saba msimu huu.
No comments:
Post a Comment