- Venue: Wembley Stadium
- Date: Friday, 6 September 2013
- Kick-off: 20:00 BST
Mshambuliaji wa Southampton Rickie Lambert atakuwa katika kikosi cha kwanza cha England kitakacho pambana dhidi ya Moldova hapo kesho baada ya Daniel Sturridge kuondolewa kikosini.
Sturridge amerejea Liverpool kwa matibabu ya mguu lakini huenda huenda akawepo safarini Ukraine.
Lambert mwenye umri wa miaka 31ambaye alifunga goli katika mchezo dhidi ya Scotland ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kuitumikia timu ya taifa ya England mwezi uliopita.
Kuelekea katika mchezo huo wachezaji Danny Welbeck na Jermain Defoe ndio washambuliaji pekee waliosalia katika kikosi cha meneja Roy Hodgson.
Wayne Rooney, Phil Jones na Glen Johnson wameondolewa kikosini tangu mapema.
Hodgson amethibitisha kuwa nahodha Steven Gerrard, Frank
Lampard na Jack Wilshere kuwa watakuwepo katika sehemu ya kiungo huku mshambuliaji nyota wa Arsenal Theo Walcott na mshambuliaji wa Manchester United Welbeck wakimsaidia Lambert wakitokea pembeni.
Sturridge mwenye umri wa miaka 24 amefunga jumla ya mabao matano ya Liverpool mapema msimu huu katika michezo mitatu ya kuanza msimu katika ligi kuu ya England.
Lambert aliifungia Southampton jumla ya mabao 15 msimu uliopita na katika msimu huu ameshafunga goli moja.
Mshambuliaji wa Manchester United Rooney anaendelea kujitibia majeraha ya kichwa
England squad to face Moldova:
Goalkeepers:
Fraser Forster, Joe Hart, John Ruddy
Defenders:
Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil Jagielka, Chris Smalling, Kyle Walker
Midfielders:
Ross Barkley, Michael Carrick, Tom Cleverley, Steven Gerrard, Frank
Lampard, James Milner, Raheem Sterling, Andros Townsend, Theo Walcott,
Jack Wilshere
Strikers:
Jermain Defoe, Rickie Lambert, Danny Welbeck, Ashley Young
No comments:
Post a Comment