On the mend: Wayne Rooney poses with a fan after
recovering from his head injury - he was back in training for the first
time today.
Nasty: Wayne Rooney's head injury kept him out of England's matches but he is now back in training.
R and R: Rooney spent the international break on holiday in the Algarve
Wary: Rooney is understood to be training on his
own away from the first team squad, with David Moyes not willing to
rush him back into action.
Wayne Rooney amerejea mazoezi katika klabu yake ya Manchester United baada ya kukosa michezo miwili ya England ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine.
Siku kumi zilizopita mshambuliaji huyo alipatwa na majeraha baada ya kugongana na mchezaji mwenzake Phil Jones, majeraha yalitopelekea kuukosa mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool ambao United walichapwa kwa 1-0 katika dimba la Anfield na pia kuwekwa nje ya kikosi cha England katika michezo miwili muhimu ya kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia.
Rooney
amerejea mazoezini na United katika uwanja wa mazoezi wa AON Training
Complex hii leo na ameenzia katika chumba cha kujenga misuli 'gym'.
Mchezaji mpya Marouane Fellaini ameanza mazoezi leo katika kikosi cha meneja David Moyes huku akitarajiwa kuanzishwa katika mchezo ujao wa Jumamosi dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Old Traford.
Inadhaniwa kuwa Rooney huenda akarejea uwanjani katika mchezo wa septemba 22 dhidi ya Manchester City katika dimba la Etihad.
Hata hivyo bado iko katika hali ya 50/50 kwa mujibu wa timu ya watabibu wa United.
Marouane Fellaini akiingia kwa mara ya kwanza katika viunga vya mazoezi vya Manchester United.
No comments:
Post a Comment