Wayne Rooney ametupia picha hii kwenye ukurasa wake wa Facebook
Rooney alikuwa na familia yake akiwemo mkewe Coleen (kulia)
Jeraha kubwa kichwani kwa mshambuliaji wa United Wayne
Rooney ambalo litapelekea kumuweka nje ya uwanja mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England katika michezo ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine limewekwa wazi.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United amepatwa na maswahibu hayo katika viunga vya Apple Jacks Adventure Park huko Warrington akiwa na familia yake akiwemo mkewe Coleen.
Rooney amepasuka kichwani kwa urefu wa nchi tatu akiwa mazoezini pale alipogongana na mchezaji mwenzake Phil Jones Jumamosi.
Mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya England Theo Walcott amesema alishituka pale aliposhuhudia ukubwa wa mpasuko wa mshambuliaji huyo.
Ananukuliwa Walcott akisema
'Nimeona picha na ni jeraha kubwa mno si vizuri kuangalia. Ni kitu kama filamu ya kutisha.'
'Nimeliona jeraha halisi na si kitu cha kukaribia kwa kweli kwa kusema kweli.
'Ni vema kwa kuwa Danny (Sturridge)
bado yupo hapa hilo ni jambo jema. Danny Welbeck ameanza msimu vizuri katika klabu yake na Rickie Lambert pia amekuwa na mwanzo mzuri wa kuanza katika kikosi cha England hivyo meneja ana chaguo zuri katika kikosi.'
Rickie Lambert (kushoto) na Danny Welbeck kulia wanapewa nafasi ya kuchukua nafasi ya majeruhi Rooney katika kikosi cha England
Timu ya watabibu wa kikosi cha England imetazama ukubwa jeraha la kupitia picha na imeamua kumuongoa kikosini Rooney kuelekea katika michezo miwili ya kufuzu.
Hodgson
atakuwa katika maombi ya kutaka Sturridge, ambaye mara tano katika michezo ya ufunguzi ya Liverpool awe fiti katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Ukraine.
Theo Walcott akiongelea juu ya michezo ya kufuzu ya England na pia juu ya jeraha la Rooney.
Katika kundi H England iko nafasi ya pili nyuma ya Montenegro kwa alama mbili na alama moja juu ya wanaoshika nafasi ya tatu Ukraine.
Mshindi mmoja ndiye atakayefuzu huku mshindi wa pili akitarajiwa kuingia katika hatua ya pili ya michezo ya mtoano yaani play-off, hivyo kuufanya mchezo huo kuwa mgumu.
Meneja wa England Roy Hodgson pichani juu anayekabiliwa na kazi ya kutafuta chaguzi nzuri kuelekea katika mchezo dhidi ya Moldova.
England head injuries are nothing new...
Mejeraha ya mchezaji wa England Terry Butcher akionekana jezi yake ikiwa imetapakaa damu katika mchezo dhidi ya Sweden mwaka 1989
Paul Ince naye alipatwa na maswahibu kama hayo akicheza kishujaa dhidi ya Italia mwaka 1997
No comments:
Post a Comment