KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 9, 2013

EXCLUSIVE: Martinez huenda akapewa mpango wa kudumu na Porto na kumtoa mikononi mwa Arsenal moja kwa moja

Poacher: Jackson Martinez was subject of interest from many English sides in the summer
 Jackson Martinez

 Porto imepiga hatua moja mbele muhimu yenye lengo la kumbakisha mshambuliaji wa Kireno kutoka katika klabu ya Arsenal kwa kumpa ofa kubwa ya kusajili kwa minajili ya mpango wa kudumu.
Jackson Martinez yuko katika rada ya mzee Arsene Wenger wakati wa usajili wa dirisha dogo la mwezi januari baada ya kuwa kufanya mambo makubwa tangu ajiunge na Porto ambapo amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 33 katika jumla ya michezo 37 aliyoichezea klabu hiyo tangu kuanza kwa msimu uliopita.
Aina yake ya umaliziaji imeonekana kuivutia Arsenal kiasi kuweka utashi wake huku Chelsea wakimuangalia kama ndio jibu sahihi la mbadala kufuatia kumkosa Wayne Rooney wakati wa kiangazi lakini puia inaarifiwa Liverpool nao kuhusishwa.
Hata hivyo Porto imejibu kwa kukaza uzi kwa hofu ya kumpoteza na kuelekea katika Barclays Premier League ambapo sasa wameanza mazungumzo ya mpango mpya wa kudumu.
Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Colombia mwenye umri wa miaka  27 atakuwa nje ya mkataba ifikapo 2016 na huenda akapewa ofa nono ya karibu asilimia 100 tofauti na ilivyo sasa ambapo inaarifiwa huenda akapewa malipo ya pauni £45,000 kwa wiki endapo Porto mabingwa wa Ureno watafanikiwa kumbakisha mpaka 2018.
Fan favourite: Martinez has built an exceptional reputation for himself both in Portugal, and Europe.
Kipenzi cha mashabiki wa Porto Martinez amejijengea sifa ndani ya Ureno na Ulaya kwa ujumla.Burden: There has been an over-reliance on Olivier Giroud at times this season at Arsenal
Olivier Giroud

Martinez pengine angesajiliwa na Rafa Benitez kuelekea Napoli, lakini timu hiyo ya Serie A iliachana na mpango wa kusajili.
Akisajiliwa kutoka katika klabu ya Chiapas ya nchini Mexico, Martinez aliongoza kwa kufunga msimu uliopita akifunga magoli 26 magoli sita mbele ya anayemfuatia Lima wa Benfica na katika msumu huu akiwa ameshapachika wavuni magoli saba.
Arsenal nao wanaamini juu ya umuhimu wake kwani uwepo wake katika safu ya ushambuliaji ambayo inamtegemea zaidi Olivier Giroud huenda ikaongeza chachu ya safu hiyo. Hata hivyo wakala wake Luis Manso kwasasa yuko katika mazungumzo na viongozi wa Porto na matumaini yao ni katika uhamisho wa mapema mwakani.

No comments:

Post a Comment