Young Africans wamerejea wamerejea jijini Dar es salaam wakitokea
kisiwani Pemba ambako walikuwa wameweka kambi ya maandalizi ya mchezo
huo.
Kikosi cha Young Africans ambacho kinashika nafasi ya nne katika
msimamo wa Ligi kikiwa na pointi 15, alama tatu nyuma ya vinara wa Ligi
Kuu ya Vodacom Simba SC kitashuka dimbani kesho jumapili kwa lengo la
kusaka alama tatu muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye
msimamo.
Young Africans ambayo
inanolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts ambaye amekaririwa na mtandao wa klabu hiyo akisema anatambua
michezo ya watani wa jadi duniani kote huwa ni migumu lakini kwa sasa
haoni sababu itakayowazuia kuibuka na ushindi katika mchezo huo japokuwa
Simba timu nzuri pia.
'Ushindi kwetu siku ya jumapili ni muhimu,
ni muhimu kwa sababu tunapigania kutetea tena ubingwa wetu kwa awamu ya
pili mfululizo, kikubwa tunawaomba wapenzi, washabiki na wanachama waje
kwa wingi kuwashangilia vijana wao watakpokuwa wanapeperusha bendera ya
watoto wa jangwnai.'
No comments:
Post a Comment