KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 21, 2013

YA SIMBA NA YANGA PICHANI.

Dakika ya 15 mshambuliaji wa timu ya Yanga Mrisho Ngassa aliyeapa hivi karibuni kuifunga timu ya Simba au kusababisha bao mapema leo, Ngassa anaunganisha krosi safi iliyopigwa na Kavumbagu hatimaye Ngassa kuunganishia mpira huo nyavuni.Dakika ya 37 Khamis Kiiza "Diego" anafunga bao la pili kwa timu yake Yanga baada ya kupata mpira kwa juu na kuumalizia ndani ya lango la Simba kufanya 0-2 dhidi ya Simba.(HISANI YA LENZI YA MICHEZO BLOG)

Dakika za lala salama za kipindi cha kwanza Khamis Kiiza akaongeza bao jingine la tatu na kuwanyamzisha mashabiki wa Simba baada ya kuwachambua mpaka mabeki wa Simba. Kipindi hicho kilichokuwa kimeongezwa dakika mbili kilimalizika Simba wakiwa na umiliki wa mpira kwa Asilimia 48 na Yanga wakiongoza kwa 52%.
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia na kumpongeza mwenzao Hamis Kiiza baada ya kutupia bao la tatu, alilofunga baada ya pasi nzuri kutoka kwa Didier Kavumbagu.
Hamis Kiiza, akishangilia bao lake la pili, alilofunga kutokana na mpira wa kurushwa na Mbuyu Twite.
Kipindi cha pili dakika ya 53  Simba wakafunga bao la kwanza bao la Mwombeki. Simba kipindi hiki cha pili wamekuja kivingine wamepata bao jingine la pili Bao la Joseph Owino dakika ya 57 baada ya kupigwa kona safi na Joseph Owino kuujaza kwa kichwa nyavuni mwa lango la Yanga na kufanikisha matokeo kuwa tofauti na kuwa 2-3.
Simba wakiwa wametoka nyuma ya bao 3-0 za Yanga wamekamliwa na bao zote tatu zikarudishwa kipindi cha pili.
Dakika 83 frii kiki iliyopigwa kwenye lango la timu ya Yanga na hatimae mchezaji Gilbert Kaze kujitwisha ndoo hadi langoni na kufanya Simba wasawazishe bao zote na kufanya 3-3.

Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Baada ya Simba kusawazisha mabao yote matatu viongozi na mashabiki wa timu hiyo walionekana kushangilia sare hiyo, ambayo kila mmoja aliyekuwapo uwanjani hapo hakuweza kuamini kilichotokea kuanzia mashabiki, wachezaji wa Yanga na hata wa Simba.

Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.

Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.

Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.

Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
Mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga, akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba na wawili wa Yanga walizimia.

Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.

No comments:

Post a Comment