Mwamuzi aliyesimamia mechi ya
Manchester City dhidi ya CSKA Moscow hafai tena kuchezesha mechi yoyote,
kwa kushindwa kuzuia matukio ya ubaguzi wa rangi uwanjani.
Toure anadai mashabiki walimtukana kwa kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi
Hayo ni maoni ya mwenyekiti wa chama cha kuzuia ubaguzi wa rangi katika soka nchini Uingereza, Kick It Out, Lord Ouseley.
Mchezaji
wa Manchester City, Yaya Toure, alikuwa amemlalamikia refa Ovidiu
Hateganabout, kufuatia kelele za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki
wa CSKA katika mechi yao ya ligi ya klabu bingwa Ulaya, na ambayo City
ilipata ushindi.
"Huyu mwamuzi hafai kuchezesha tena mechi," aliielezea BBC.
"Alishindwa kutekeleza wajibu wake usiku wa jana, na hili ni suala wazi ambalo Uefa inafaa kupambana nalo."
Kufuatia muongozo ambao ulitolewa na shirikisho
la kusimamia soka la Ulaya, Uefa, mwaka 2009, waamuzi wana mamlaka ya
kusitisha matamshi ya ubaguzi wa rangi uwanjani kutoka kwa mashabiki.
Mwamuzi, kama hatua ya kwanza, anaweza kusitisha mchezo, na kuamuru kutumia vipaaza sauti uwanjani katika kuwaonya mashabiki.
Kati ya hatua ambazo zimetekelezwa na Uefa dhidi
ya vilabu vilivyohusika katika matukio ya ubaguzi wa rangi ni pamoja na
kuwafungia mashabiki viwanja vya Dinamo Zagreb ya Croatia, Legia Warsaw
ya Poland na Honved ya Hungary.
Uwanja wa Lazio pia ulikuwa umefungwa kabisa, lakini baada ya kukata rufaa, kwa kiasi fulani mashabiki waliruhusiwa tena.
Viwanja ambavyo bado havijafunguliwa kikamilifu
kwa mashabiki ni vile vya Poland, Lech Poznan na Piast Gliwice, na vile
vya APOEL Nicosia ya Cyprus na HNK Rijeka ya Croatia.
Hatua ya pili ya mwamuzi ni kuusimamisha mchezo kwa muda, na rabsha za ubaguzi wa rangi zikiendelea, kuisimamisha mechi kabisa.
Kwa kuwa Toure aliripoti matukio hayo kwa
mwamuzi wakati wa mechi, na pia kuzungumza naye baadaye, tukio hilo
litaandikishwa katika ripoti rasmi ya mechi, na kufikishwa Alhamisi kwa
Uefa.
Manchester City, kama klabu, pia imewasilisha malalamiko hayo kwa Uefa.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC mjini Moscow, Steve
Rosenberg, anasema klabu ya CSKA Moscow inadai kwamba Toure peke yake
ndiye alizisikia kelele hizo za ubaguzi wa rangi.
No comments:
Post a Comment