ROCK CITY MARATHON 2013 REKODI YAVUNJWA MATUKIO PICHANI.
Mshindi
wa kwanza wa mbio za Rock City Marathon 2013 kilomita 21 kwa upande wa
wanaume Alphonse Felix kutoka mkoani Arusha akimalizia mbio hizo kwenye
uwanja wa CCM Kirumba ambapo alitumia saa 1:02:17 na kufanikiwa kuvunja
rekodi iliyowekwa mwaka jana na Opio Chacha aliyetumia saa 1:05:47. Afisa
Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF Bi. Theopista
Mheta akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,500,000/= mshindi wa kwanza mbio
za Rock City Marathon kilomita 21 kwa upande wa wanaume Alphonse Felix
ambaye pia alijinyakulia zawadi ya tiketi ya ndege toka moja wa
wadhaamini wa mbio hizo Pecision Air ya kuelekea jijini Dar es salaam na
kurudi mkoani kwake Arusha
No comments:
Post a Comment