|
Rais Mpya Jamal Malinzi (kulia) akipokea katiba ya TFF toka kwa Rais anayemaliza muda wake Leodgar Tenga |
|
Hapa akikabidhiwa mpira. |
|
Kamati ya uchaguzi ikikamilisha kazi |
|
Uongozi mpya wa TFF |
|
Ayub Nyenze akiwa ameshikiliwa na madaktari baada ya presha kupanda kwa furaha ya ushindi |
|
Athuman Nyamlani akiondoka ukumbini mapema saa tatu baada ya kusikia fununu kuwa kashindwa |
|
Wapambe wa Malinzi wakipongezana baada ya kusikia ushindi wa Malinzi |
|
Wajumbe wakifuatilia matokeo ukumbini hapo ni Linna Kessi mjumbe mpya na Simon Nyala aliye angushwa |
|
Tenga akiwa na Mamelod (katikati) na Tandau |
|
Hapa wajumbe wamechoka hadi wanasinzia |
|
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi mpya |
KATIKA
kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa TFF, uliofanyika jana na kumalizika
alfajiri ya leo, Jamal Emil Malinzi,amefanikiwa kuibuka kidedea na kuwa
Rais mpya wa Shirikisho hilo baada ya kuibuka na jumla ya Kura, 72
dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika
uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es
Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa
kupata jumla ya kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani aliyeibuka na kura
52 na Imani Madega, aliyepata 6.
Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13;
kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda
Muhsin Said aliyepata kura 50, Omar Abdulkadir, kura 10 na Alex
Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.
Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda
Riziki Majala aliyepata kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto
kura 26 na Farid Mbaraka kura 14.
Aliyeshinda Kanda ya 10 ni Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata kura nne na Stewart Nasima kura 58.
Kanda ya 9, Othman Kambi aliyepata kura 84 ndiye aliyewashinda wapinzani wake, Francis Bulame aliyepata kura kura 30 na James.
Baada ya kutangazwa Jamali alitoa
shukurani na kuvunja kamati zote za TFF na kuwasamehe waamuzi wote
waliofungiwa kwa makosa ya kawaida isipokuwa wale waliofungiwa kwa
makosa ya rushwa.
No comments:
Post a Comment