Inter Milan inajipanga kumsajili nahodha wa zamani wa Arsenal Thomas Vermaelen wakati wa kipindi cha usajili cha mwezi Januari.
Vermaelen, ambaye alishuka kiwango Emirates Stadium, ameshacheza mchezo mmoja tu msimu huu.
Baada ya pendekezo langu la mwezi uliopita kuwa huenda akaihama Arsenal
kusaka nafasi ya kucheza huko nchini Belgium katika kombe la dunia, Inter Milan imechomoza kutaka huduma yake.
Kikosi hicho kinachoshiriki ligi kuu ya soka nchini Italia baada ya kuchukuliwa na mfanya biashara kutoka nchini Indonesia
Erick Thohir kimesema kuwa Vermaelen ni miongoni mwa mawindo ya klabu hiyo.
Klabu hiyo inadhani hilo litakuwa ni jaribio kwa Arsenal watakapo weka ofa yao ya pauni milioni £8 lakini wamesema huenda wakafikia mpaka ofa ya pauni milioni £10 kujaribu kufanikiwa kunasa saini ya kiungo huyo.
Arsene Wenger amekaririwa kabla ya mchezo wa leo dhidi ya Crystal
Palace mbele ya waandishi wa wa habari akisema "skipper' huyo hafurahii maisha huko London ya Kaskazini na kumtaka kuwa mvumilivu
Vermaelen ana mkataba na Arsenal mpaka 2015.
No comments:
Post a Comment