Vilabu vya kabumbu nchini Ufaransa vitafanya mgomo mwezi ujao wa Novemba
kwa mara ya kwanza katika miaka 40 kulalamikia mipango ya serikali
kuwatoza kodi ya asilimia 75 wanaopata mapato makubwa.
Mgomo huo wa kwanza katika soka la Ufaransa tangu mwaka wa 1972
unatarajiwa kuandaliwa katika wikendi ya mwisho ya Novemba baada ya
vilabu vya nchini humo kupiga kura kwa kauli moja dhidi ya mpango huo
wenye utata wa Rais Msoshalisti wa Ufaransa Francois Hollande wa kutoza
kiwango kikubwa cha kodi.
Rais wa chama cha vilabu vya soka vya Ufaransa – UCPF Jean-Pierre Louvel
amesema hakutakuwa na mechi mnamo tarehe 29 Novemba na Desemba 2. Chini
ya mapendekezo hayo, makampuni badala ya wachezaji yatahitajika kulipa
kiwango cha juu cha kodi kwa niaba ya wafanyakazi waoambao ni wachezaji
ambacho kinazidi euro milioni moja.
Louvel anasema vilabu ambavyo vina wasiwasi kuwa uwezo wao wa kuwavutia
wachezaji mahiri wanaopata mishahara minono kutoka ng'ambo kucheza
nchini Ufaransa utakwama, vitafungua milango yao kwa mashabiki kufafanua
kwa wafuasi wao ni kwanini wanahitaji kuchukua hatua hizo kali.
No comments:
Post a Comment