Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) limesema kuwa droo ya michuano ya msimu huu itafanyika wiki ijayo jijini Nairobi.
Katibu wa baraza hilo Nicholas Musonye, amenukuliwa na vyombo vya habari vya Kenya akisema wanafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kufannikisha michuano hiyo ambayo itafanyika katika miji ya Mombasa, Nairobi na miji mingine miwili ambayo itathibitishwa na waandaaji.
“tunasubiri uthibtisho kutoka kwa nchi wanachama na tunataka kukuhakikishia tutaandaa vya mafanikio",
Mabingwa watetezi Uganda Cranes are kwasasa wanajipanga kwa mchezo wa kirafiki Novemba 16 dhidi ya Rwanda katika uwanja wa Namboole Stadium kama sehemu ya maandalizi yao chini ya Msebia Milutin Sedrojevic.
Tayari Mombasa wamethibtisha kuwa wenyeji wa kundi moja baaa ya meya wa jiji hilo Hassan Ali Joho kuwasilisha kwa Local Organising
Committee (LOC) kuwa wako tayari.
Michuano hiyo itakuwa iankwenda sambamba na sherehe za uhuru za miaka 50 ya Kenya.
Tayari UBC wamethibtisha kuyarusha moja kwa moja.
Somalia imetangaza kikosi kwa ajili ya michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanzaNovemba 27 na kumalizika Desemba 12.
No comments:
Post a Comment