KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 8, 2013

IVORY COAST KUMKOSA CHEICK TIOTE MCHEZO DHIDI YA SENEGAL

Kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi jana alitangaza kikosi cha wachezaji 25 kabla ya kuikabili Senegal katika mchezo wa mkondo wa pili kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia (playoff game) uliopangwa kufanyika Novemba 16 katika mjini mkuu wa Morocco ambapo amemuacha kiungo wa Newcastle Cheick Tiote baada ya kusimamisha.
Nyota wa FC Bale Geoffrey Serey Die pia anakabiliwa na adhabu ya kusimamishwa ambapo sasa wamejumuishwa mshambuliaji wa CSKA Moscow Seydou Doumbia na Mathis Bolly wa Fortuna Dusseldorf.
Gervinho, ambaye hivi karibuni amerejea mazoezini katika klabu yake ya Roma baada ya kuwa majeruhi pia amejumuishwa katika orodha ya wachezaji wa kikosi hicho huku pia mkongwe Didier Drogba na kiungo nyota Yaya Toure pamoja na Kolo Toure na Salomon Kalou wakijumuishwa.
Tembo hao wa Ivory Coast waliawachapa simba wa milima ya Teranga 3-1 katika mchezo uliopigwa mwezi uliopita mjini Abidjan.
Kocha wa Senegal Alain Giresse amewaambia wanahabari kuwa wakati wa kutangaza kikosi kuwa ana matumaini ya kubadili matokeo ya mchezo uliopita na kupata tiketi ya kucheza kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
 Kikosi
Goalkeepers: Boubacar Barry (Lokeren, Belgium), Sylvain Gbohouo (Sewe Sport), Abdoul Karim Cisse (Africa Sports).
Defenders: Kolo Abib Toure (Liverpool, England), Benjamin Angoua (Valenciennes, France), Serge Aurier (Toulouse, France), Souleman Bamba (Trazbonspor, Turkey), Arthur Boka (Stuttgart, Germany), Viera Diarrassouba (Caykur Rizespor, Turkey), Jean Daniel Akpa Akpo (Toulouse, France), Didier Zokora (Trazbonspor, Turkey).
Midfielders: Jean-Jacques Gosso-Gosso (Glençlerbirligi SK, Turkey), Ismael Diomande (Saint-Etienne, France), Max-Alain Gradel (Saint-Etienne, France), Abdul Razack (Anzhi, Russia), Koffi Romaric Ndri (Bastia, France), Yaya Toure (Manchester City, England).
Forwards: Lacina Traore (Anzhi, Russia), Wilfried Bony (Swansae, England), Gervinho (AS Roma, Italy), Didier Drogba (Galatasaray, Turkey), Salomon Kalou (Lille, France), Giovanni Sio (FC Bale, Switzerland), Mathis Bolly (Dusseldorf, Germany), Seydou Doumbia (CSKA Moscou, Russia).

No comments:

Post a Comment