KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 8, 2013

PSG wajiandaa kudhibiti uongozi

Baada ya kukashifu vijana wake kwa kulegeza kamba kwenye Ligi ya Mabingwa, kocha wa Paris Saint-Germain, Laurent Blanc anatazamia ubora zaidi wakati watakapoalika Nice katika uwanja wa Parc des Princes Jumamosi.
PSG walikosa nafasi ya kufuzu raundi ya muondoano baada ya kutoka sare 1-1 na Anderlecht Jumanne lakini matokeo hayo yalihifadhi hadhi yao ya kutoshindwa musimu huu katika mashindano yote.
Sasa, wanadhamiria kuongeza mwanya kati yao na wapinzani wa karibu Lille na Monaco katika kilele cha Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.
Mwaka unakaribia tangu klabu hicho kuchakazwa nyumbani na wana zana za kuwafurusha Nice waliomo nafasi za kati katika jadwali ambao wamepoteza mechi tatu kati ya nne za mwisho.
Blanc anatarajiwa kumkaribisha tena Edinson Cavani ambaye amezamisha mabao tisa kwenye ligi baada ya kukosa mvutano dhidi ya Anderlecht huku nahodha Thiago Silva pia akishiriki baada ya kurejea baada ya mwezi mmoja katika sare hiyo.
“Nilitaka ashiriki lakini kwa mpangilio tofauti na ikiwa tulitaka acheze dhidi ya Nice, ni lazima angepishwa katika mechi ya Anderlecht,” Blanc alielezea kuhusu kinara wake uwanjani.
Nice wana matatizo langoni huku David Ospina, anayechezea kikosi cha taifa cha Colombia, akikosa mchezo kwa wiki sita na jeraha la goti huku kiungo wake wa ziada, Mouez Hassen akibakia nje pia.
Hayo yamefanya chipukizi Luca Veronese, 22, kutumika kama kipa kwa mara ya kwanza Ligue 1.
Monaco wanatazama kukausha machozi ya kushindwa 2-0 ugenini Lille, mara yao ya kwanza kuonja kichapo, watakapoalika Evian katika uga wa Stade Louis II Ijumaa.

No comments:

Post a Comment