Kocha wa timu ya soka ya Wales Chris Coleman
atakutana na maafisa wa chama cha soka cha Wales hii leo kujadili kuhusu
mkataba mpya.
Coleman ambaye mkataba wake unamalizika baada ya
mchezo kati ya Wales na Finland tarehe 16 mwezi Novemba, ameelezwa
kupigiwa pande kuziba nafasi iliyo wazi kwenye timu ya Crystal Palace
Tetesi kuhusu mustakabali wa Coleman
ziliongezeka baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa waandishi wa habari
hii leo uliokuwa umelenga kutaja kikosi kitakachovaana na Finland, huku
maafisa wa Wales wakisema kuwa wamejadiliana na Chris na kuamua kuwa
watataja kikosi hicho kwa njia ya barua pepe.
Msemaji wa chama cha mpira cha Wales amesema
kuwa wanaona kuwa zoezi la kuita mkutano wa waandishi wa habari
hautakuwa na maana kwa kuwa maswali yatajielekeza kuhusu mkataba wa
Chris na mipango ya kuhamia Crystal Palace.
Klabu ya crystal Palace ambayo Coleman amekuwa
akiichezea kwa miaka minne imekuwa ikitafuta Kocha mpya baada ya
kuondoka kwa Ian Holloway kuondoka mwezi uliopita.
Mkataba mpya wa Coleman utakuwa kwenye ajenda
katika mkutano kati yake na maafisa wa Chama cha soka cha Wales zikiwa
zimebaki siku nane pakee kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika.
No comments:
Post a Comment