![]() |
Lina Kessy |
TANZANITE YATUA SALAMA MAPUTO
Kikosi
cha timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili
salama jijini Maputo, Msumbiji tayari kwa mechi ya marudiano ya raundi
ya kwanza ya Kombe la Dunia itakayochezwa kesho (Novemba 9 mwaka huu).
Kwa
mujibu wa kiongozi wa msafara wa Tanzanite, Kidao Wilfred ambaye pia ni
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), timu hiyo chini ya Kocha wake Rogasian Kaijage ilifanya mazoezi
yake ya kwanza jana asubuhi.
Tanzanite
itafanya mazoezi yake ya mwisho leo (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi hiyo
itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa za Msumbiji.
Nao
wachezaji waliobaki kumalizia mtihani yao ya kidato cha nne wameondoka
leo saa 11 jioni kwa ndege ya LAM wakiongozwa na naibu kiongozi wa
msafara, Khadija Abdallah Nuhu ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA).
KESSY KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Lina Kessy kuwa kamishna wa
mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa
miaka 20 kati ya Afrika Kusini na Botswana.
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Afrika Kusini,
Novemba 9 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zambia ndiyo watakaochezesha mechi
hiyo namba kumi.
Waamuzi
hao wataongozwa na Glads lengwe atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi
msaidizi namba moja ni Bernadette Kwimbira kutoka Malawi, namba mbili ni
Mercy Zulu na mezani atakuwepo Sarah Ramadhani, wote wa Zambia.
Afrika
Kusini ilishinda mechi ya kwanza ugenini mabao 5-2. Mshindi wa mechi
hiyo atacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi kati ya Tanzania na
Msumbiji.
No comments:
Post a Comment