Mechi za mchujo za kufuzu katika Kombe la Dunia nchini Brazil zinarudi
tena, ambapo Ufaransa inakabiliwa na jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa
haikosi nafasi ya kushiriki katika michuano hiyo tangu miaka 20
iliyopita.
Hakuna timu yoyote ya Ulaya ambayo imewahi kufuzu kwa Kombe la Dunia
kupitia mechi za mchujo, baada ya kushindwa mkondo wa kwanza magoli
mawili kwa sifuri.
Ufaransa iliduwazwa na Ukraine kwa kufungwa mabao
mawili bila jawabu Ijumaa iliyopita, hiyo ikiwa na maana kuwa vijana hao
wa kocha Didier Deschamps watahitaji kuonyesha mchezo wa kiwango cha
juu katika mchuano wa marudiano hapo kesho.
Baada ya kushinda raundi ya kwanza ya vita kati yake na Zlatan
Ibrahimovic wakati alipopachika wavuni bao la kichwa na lililoipa Ureno
ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Sweden, Christiano Ronaldo ana
matumaini kuwa anaweza tena kuwa shujaa katika uwanja wa kitaifa wa
Sweden hapo kesho. Zlatan alishindwa kutamba mjini Lisbon na anataraji
kuwa mambo yatakuwa tofauti katika mkondo wa pili.
Ugiriki wako katika
nafasi nzuri baada ya ushindi wao wa mabao matatu kwa moja dhidi ya
Romania katika mkondo wa kwanza, wakati nao Iceland wakiyaweka hai
matumaini yao ya kushiriki kwa mara ya kwanza kabisa katika Kombe la
Dunia baada ya kulazimisha sare ya kutofungana goli dhidi ya Croatia.
Khedira auguza jeraha la goti
Huenda ukawa ni mchezo tu wa kirafiki wa kujipima nguvu na pia
kuwapa wakocha wa timu zote mbili fursa ya kuvitathmini vikosi vyao
na kujua uwezo wa wachezaji, lakini pia, mechi ambayo inawaleta pamoja
watani wa jadi.
Matarajio ya Uingereza, ya kufanya vyema katika kombe la dunia kombe la dunia
yatamulikwa tena hapo keshi wakati watakaposhuka dimbani dhidi ya watani wao
wa jadi Ujerumani katika uwanja wa nyumbani Wembley.
Vijana hao wa Kocha
Roy Hodgson waliduwazwa na Chile Ijumaa iliyopita kwa kurambishwa
magoli mawili kwa sifuri, kikiwa ni kichapo chao cha kwanza katika mechi
10 za mwisho.
Matayarisho ya kocha wa Ujerumani Joachim Löw siyo tu kwa mchezo huo
bali kwa michuano ya kombe la dunia wiki iliyopita yalipata pigo kutokana
na habari za jeraha la Sami Khedira.
Kiungo huyo wa Real Madrid
alifanyiwa upasuaji wa jeraha la goti na huenda akawa mkekani kwa miezi
sita.
Kocha Löw alielezea matumaini kuwa nyita huyo huenda akapona
katika muda unaofaa kabla ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
"Tumehuzunishwa kwa
sababu katika miaka yangu ya nyuma, tangu mwaka wa 2004, nikiwa hapa
sikumbuki kama pamewahi kutokea jeraha baya kama hili.
Na kwa Sami
ambaye kwetu ni mchezaji muhimu, jeraha lake ni pigo kwetu"
Ujerumani ilitoka sare ya goli moja kwa moja na watani wao Italia
Ijumaa.
Kando na Khedira, wachezaji wawili wa Bayern Munich Nanuel Neuer
na Philipp Lahm, nahodha, pia wameachwa nje ya kikosi kitakachopambana
na England.
Pia Löw amempumzisha mchezaji wa Arsenal Mesut Özil. Mlinda
lango wa Borussia Dortmund Roman Weidenfeller atavaa glovu za Neuer.
Löw anasema "Franz Beckenbauer aliwahi kusema “tunauita mchuano wa
mafahali wawili.
Kucheza uwanja wa Wembley ni kitu kizuri sana mbele ya
mashabiki 80,000 au 85,000. hiyo pekee ni motisha ya kutosha na
Uingereza bado ni mojawapo ya timu kubwa".
No comments:
Post a Comment