Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu – Amnesty
International limeshutumu “kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa
wafanyakazi wa ujenzi nchini Qatar, kwenye ripoti yake ya hivi punde.
Amnesty Internationa imeitaka Qatar kuitumia fursa ya kuandaa dimba la
Kombe la Dunia mwaka wa 2022 kwa kuonyesha kuwa imejitolea kulinda haki
za binaadamu. Ripoti ya Amnesty International inasema wafanyakazi wa
kigeni wanaishi kama “wanyama“, neno ambalo shirika hilo limesema
watafiti wake walimsikia mkurugenzi mmoja wa kampuni ya ujenzi
akilitumia kuwaelezea wafanyakazi hao.
Salil Shetty ni Katibu Mkuu wa Amnesty International na anasema "Kitu
kimoja ambacho tunaamini kinapaswa kutatuliwa haraka ni mfumo wa kutoa
vibali vya kuondoka. Tunadhani hilo linastahili kushughulikiwa haraka.
Matatizo ya ukiukaji wa haki za binaadamu kuhusiana na wafanyakazi wa
kigeni nchini Qatar ni makubwa mno. Yamesambaa kote. Siyo matukio
machache tu".
Serikali ya Qatar inapinga madai hayo kuwa inawanyanyasa wafanyakazi wa
kigeni, ikisema itayaijumuisha ripoti hiyo katika uchunguzi ambao tayari
ilianzisha. Nasser al-Khater kutoka kwa kamati ya Kombe la Dunia 2022
nchini Qatar anasema nchi hiyo inajaribu kurekebisha sheria hizo….."ni
nchi inayokuwa kwa kasi sana kwa idadi ya watu, na mojawapo ya nchi
zinazokuwa kwa kasi kiuchumi ulimwenguni, hivyo ni wazi vitu haviwezi
kuimarika kwa wakati mmoja."
Ripoti hiyo imetoa wito kwa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA
kulishinikiza taifa hilo la Guba kuimarisha mazingira ya wafanyakazi wa
kigeni, wengi wao ambao wanatokea Kusini au Kusini mashariki mwa Asia.
Wafanyakazi hao wanalalamika kutolipwa mishahara yao, mazingira magumu
na hatari ya kufanyia kazi, na viwango vya kushutusha vya malazi. Wengi
wao wamekwama nchini Qatar wasiweze kuondoka. Wafanyakazi wengi pia
wameripoti hali mbaya ya afya na viwango duni vya usalam
No comments:
Post a Comment