KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, November 18, 2013

STEVEN GERRARD KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA BAADA YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL.

Steven Gerrard ametanabaisha kuwa anafikiria kuachana na soka la kimataifa baada ya fainali ya kombe  la dunia kiangazi ijayo.
Nahodha huyo England amekuwa katika kikosi cha kwanza katika timu zote akiwa pia ni nahodha kwa zaidi ya muongo mmoja na msimu huu akicheza jumla ya michezo 18 mashondano yote.
Gerrard atakuwa na umri wa miaka 34 wakati michuano ya kombe la dunia itakapo kuwa inafanyika nchini Brazil amesema mwili wake unahitaji kupumzika hapo baadaye.

‘hamu na mahitaji ya kuendelea ipo, nahitaji kucheza kwa muda mrefu kadri niwezavyo lakini wakati mwingine katika uchezaji wako inabidi usikilizie mwili wako na utathmini hali halisi.

 ‘Nadhani ni jambo la kuelekea Brazil na kufanya kilicho bora kwa uwezo wangu wote na mashindano yatakapo kamilika nitajadili na watu wangu wa ukweli ambao wamenisaidia kufika hapa halafu nitafanya maamuzi’

No comments:

Post a Comment