Kocha
 Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 
watakaoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya 
kuanzia Novemba 27 mwaka huu.
Kilimanjaro
 Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan
 Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu 
itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye 
Uwanja wa Machakos.
Wachezaji
 wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi 
(Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki 
ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin 
Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo
 ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), 
Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan 
Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu
 ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa 
(Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata
 (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP 
Mazembe, DRC).
Kilimanjaro
 Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda 
Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na 
kumalizika Desemba 13 mwaka huu.   
 

No comments:
Post a Comment