KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 27, 2013

Zanzibar Heroes waanza vema michuano ya Chalenji huko Nairobi.


Timu ya taifa ya Zanziba 
'Zanzibar Heroes' imeanza vema michuano ya GOtv 2013 CECAFA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya  Sudan Kusini mchezo uliofanyika katika dimba la Nyayo jijini  Nairobi.

Suleiman Kassim na Adeyum Saleh ndio waliokuwa wafungaji wa mabao hayo na hivyo kuwapa uongozi wa kundi A baada ya kukusanya alama tatu muhimu za mwanzo.

Suleiman alifankiwa kuandika bao hilo kunako dakika tano baada ya mlinda mlango wa Sudani Kusini maarufu kama 'Bright Stars’ Jumma Genaro kutokuwa na maamuzi mazuri wakati wa upigwaji wa krosi ambayo ilizamishwa nyavuni kirahisi na Selemani Kassim.

Bao hilo liliwaamsha Sudani Kusini ambao hii ni mara ya pili kushiriki michuano hiyo ya mataifa ya ukanda wa mashariki na kati ya Afrika ambapo waliweza kutawala mchezo kila eneo lakini walishindwa walishindwa kuuzamisha mpira wavuni katika lando la Heroes lililokuwa chini ya Rashid Abdallah.

Baaba ya mapumziko Sudani ya kusini iliendelea kutawala mchezo ambapo mara mbili walikaribia kuswazisha lakini Abdallah alikuwa vema langoni na kuokoa mipira ya akina Khamis Leyano ilhali Jacob Osulu akishindwa kufunga nafasi ya wazi kwa kichwa kilichokwenda upande.

Zanzibar waliweza kuandika bao la pili kunako dakika ya 67 pale ambapo Adeyum Saleh Ahmed alipopiga mpira wa kunyanyua kistaadi yaani 'volley' nyuma ya mlinda mlango Genaro.

Mabadiliko ya kumuingiza Fabiano Lako kwa upande wa Sudan Kusini yaliwapa nguvu na kuandika bao la kufutia machozi.
Goli hilo lilikuwa la kwanza katika Sudan Kusini katika michuano ya CECAFA kwani itakumbukwa katika michuano ya mwaka jana jijini Kampala walishindwa kuandika hata goli moja .
Wakati wenyeji Kenya wakilazimishwa sare ya bila mabao na Ethiopia katika mchezo mwingine matokeo hayo yanaifanya  Zanzibar kukalia usukani kwa alama zao 3 Kenya na Ethiopia wakiwa na alama moja kila mmoja na Sudan Kusini wakiwa mkiani.

No comments:

Post a Comment