KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 9, 2013

Alex Song anasema maisha yake ndani ya Camp Nou, Fabregas ni zaidi ya kaka.


 Kiungo wa Barcelona Alex Song amesema kuwa Cesc Fabregas amekuwa kama kaka yake baada ya kumsaidia kuelekeza maisha yake Camp Nou.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Cameroon alijiunga na Blaugrana kwa uhamisho uliokuwa na thamani ya euro milioni €18 wakati wa majira ya kiangazi mwaka 2012 na tangu wakati huo ameichezea michezo katika kikosi cha kwanza 22.
Hta hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema bado hayatulia ndani ya Catalonia na kuongeza kuwa kiungo mwezanke wakati huo wakiwa Arsenal Cesc Fabregas alifanya kazi kubwa kumsaidia kujisikia kama yko nyumbani.
"Ukilinganisha na mwaka wangu wa kwanza sasa najisikia faraja zaidi" Song amenukuliwa na AS.
 "unapoelekea katika nchi mpya na kuanza kujifunza lugha mpya lakini utakiwa kujifunza utamaduni mpya inahitaji muda.
"nilichokgundua hapa ni kwamba ni kama familia kubwa na kila mtu alinipokea kwa mikono miwili.
"Cesc (Fabregas) ni kama kaka kwangu. alinishika mkono na kuniongoza kwenye magumu yote tangu awali na hilo lilinifanya nijisikie vizuri zaidi.
"sasa naelewa lugha kiasi fulani licha ya kwamba bado napambana kujielezea . Maisha ni bora zaidi ninafuraha kuwepo hapa."
Song alikosolewa vibaya na bosi wake Gerardo Martino baada ya mchezo wa ushindi wa mabao 4-1 wa Copa del Rey ijumaa iliyopita dhidi ya Cartagena, ambapo kocha muajentina hakufurahishwa na kushindwa kuelewa kwa kiungo huyo juu ya majukumu yake kama kiungo.

No comments:

Post a Comment