KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 9, 2013

Ronaldo na Messi waongoza orodha ya wachezaji wanao wania Fifpro World XI

Ronaldo and Messi lead World XI shortlist

Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wameongoza uteuzi wa kikosi cha fifa cha orodha ya wachezaji 11 ( Fifa's World XI shortlist) ambapo pia washambuliaji wengine 13 wakiwemo mshambuliaji wa Paris Saint-Germain  Zlatan Ibrahimovic pia wamependekezwa.

Ronaldo na Messi ni wawili kati ya wachezaji wanne waliotajwa kutoka La Liga, huku Diego Costa na Neymar toka nchini Hispania wakiwa katika nafasi za juu kutoka vilabu vya Atletico Madrid na Barcelona.

Luis Suarez, Robin van Persie, Sergio Aguero na Wayne Rooney wanawakilisha ligi kuu ya England Premier League, ilhali Mario Mandzukic na Robert Lewandowski wakitokea katika ligi kuu ya nchini Ujrumani Bundesliga na kufanya orodha kuwa na watu 15.

Nyota wa Paris Saint-Germain  Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani wakitokea ligi ya Ufaransa Ligue 1 sambamba na mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao, huku Mario Balotelli akiwa ni pekee kutoka ligi kuu ya Italia Serie A.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Cote d'Ivoire Didier Drogba ndiye mshambuliaji pekee ambaye hachezi katika vilabu vikubwa vinavyochezea ligi kubwa tano za Ulaya.

Kikosi cha Fifpro World XI kitatangazwa wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo ya fifa ya Ballon d'Or mjini Zurich  January 13.

Fifpro World XI Shortlist of Attackers:

Sergio Aguero (Argentina, Manchester City); Mario Balotelli (Italy, Manchester City/AC Milan); Edinson Cavani (Uruguay, Napoli/Paris Saint-Germain); Diego Costa (Spain, Atletico Madrid); Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid); Didier Drogba (Cote d’Ivoire, Shanghai Shenhua/Galatasaray); Radamel Falcao (Colombia, Atletico Madrid/Monaco); Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris Saint-Germain); Robert Lewandowski (Poland, Borussia Dortmund); Mario Mandzukic (Croatia, Bayern Munich); Lionel Messi (Argentina, Barcelona); Neymar (Brazil, Santos/Barcelona); Wayne Rooney (England, Manchester United); Luis Suárez (Uruguay, Liverpool); Robin van Persie (Netherlands, Manchester United).

No comments:

Post a Comment