KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 19, 2013

Ashley Cole avamia bata la krismass la wapinzani wao wa Jumatatu Arsenal huko London.

Wote kwa pamoja wakipozi kwa ajili ya picha kabla ya kutokea kwenye bata la Christmas bash
Ashley Cole wa Chelsea aliungana na wachezaji wa timu pinzani ya Arsenal wakati Gunners wakisheherekea pati yao ya Christmas usiku wa jana licha ya kwamba Chelsea wanaandaa pati yao maarufu kama 'festive bash'.

Inaaminika kuwa mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal aliwafuaata washikaji zake akina Ryan Bertrand na Andre Schurrle huko jijini London 'Nightspot Libertine' ikiwa ni masaa 24 baada ya mchezo wao wa Capital One dhidi ya Sunderland.

Wachezaji wa Chelsea wao waliaamua kuahirisha pati yao ya Christmas ambayo pia ilitakiwa kufanyika usiku wa jana.

 Ashley Cole akijichanganya na wachezaji wa Arsenal kufuatia pati yao ya Chelsea kuahirishwa.
 Kieran Gibbs akizungukwa na ladies
 Chelsea wataumana na Arsenal katika dimba la Emirates Jumatatu mchezo ambao huuwenda ukakiweka kikosi cha Mourinho katika usukani wa msimamo wa ligi ya England.

No comments:

Post a Comment