KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 19, 2013

Pigo kwa Manchester United, Andre Iniesta aongeza mkataba Barcelona


Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta ameingia mkataba wa nyongeza na kigogo cha Hispania Barcelona kwa kusaini miaka miattu mingine ya ziada.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 sasa atasalia ndani ya klabu hiyo mpaka 2018.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika katika kipindi cha miezi 18 ijayo ambapo taarifa zilikuwa zikiarifu kuwa Manchester United ilikuwa ni moja ya klabu iliyokuwa ikinyemelea kandarasi yake mwezi Januari au wakati wa majira ya kiangazi kwa lengo la kuimarisha sehemu yake ya kiungo.

Rais wa Barca andro Rosell amethibtisha kuwa mchezaji huyo atasalia Nou Camp mpaka June 2018.

Iniesta ameichezea Barca jumla ya michezo 479 baada ya kujiunga nayo akitokea Albacete akiwa na umri wa miaka 12 mwaka 1996. Ameshinda ligi ya vilabu bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara sita.
On top of the world: Iniesta helped Spain win the World Cup in 2010 by scoring the winner in the final
Iniesta aliisaidia Hispania kutwa kombe la dunia 2010 .

Kiungo huyo wa Hispania ameifungia Barca magoli 48 na kuwa msaada katika kikosi tangu alipoaanza kucheza kama mchezaji wa kutumainiwa October 2002, ameisaida Brca kushinda jumla ya mataji 16 katika kipindi cha miaka mitano na nusu iliyopita

Sherehe za usajili wake zitafanyika Jumatatu Nou Camp.