KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 7, 2013

Mrisho Ngasa na Ivo Mapunda waipeleka Kili Stars nusu fainali ya michuano ya Chalenji.

Licha ya kutoka nyuma kimatokeo na kusawazisha bao kwa kufanya matokeo kusomeka 2-2 bado timu ya taifa ya Uganda imeshindwa kusonga mbele dhidi ya kikosi kilichokuwa na wachezaji 10 uwanjani Kilimanjaro Stars katika michuano ya  CECAFA ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa manispaa ya mji wa Mombasa ulianza kwa kusimama kwa kimya kuomboleza msiba wa simba wa Afrika mzee Nelson Mandela, aliyefariki dunia usiku wa Alhamisi huko nchini Afrika Kusini.
Shukrani kwa mabao mawili ya mshambuliaji hatari Mrisho Khalfani  Ngassa ambaye mbali ya kuandika bao la kusawazisha lakini pia aliongeza bao la pili kunako dakika za 18 na 39 katika nusu ya kwanza ya mchezo.
Uganda Crane ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi kupitia kwa Dan Sserunkuma aliyefunga goli hilo kunako dakika ya 16 baada ya kupokea mpira uliopigwa na Hamisi Kiiza kutoka winga ya kulia.
Bao la kusawazisha la Uganda lilifungwa na mlinzi Martin Mpuga kunako dakika 73.
Katika mipigo ya penati nyota wa Kilimanjaro Stars waliozamisha mipira yao nyavuni ni pamoja na Patrick Kelvin Yondani, Erasto Edward Nyoni, Frank Raymong Domayo huku  Amri Ramadhan Kiemba na Mbwana Samatta penati zao zikishindwa kuingia nyavuni.
Penati za Uganda Cranes zilizo zama wavuni zilifungwa na Hamisi Diego Kiiza na Emmanuela Okwi huku penati za kiungo Aucho Khalid wa Gor Mahia amnaye alifunga bao la kusawazisha penati kuokolewa na mlinda mlango wa Kili Stars Ivo Mapunda.
 
Kilimanjaro stars ilicheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa takribani dakika 30 katika kipindi cha pili kufuatia kiungo wake Salum Abubaker kutolewa nje na mwamuzi Msomali Wish Yabarow.

Uganda: Benjamin Ochan (GK), Nicholas Wadada , Geofrey Walusimbi , Richard Kassaga, Martin Mpuga , Khalid Aucho ,Joseph Mpande , Geofrey 'Baba' Kiziito,Dan 'Muzei' Sserukuma, Hamis 'Diego' Kizza, Emma Okwi.

Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo

TANZANIA:
Phillip Ivo Mpunda (GK),Kelvin Yodani ,Erasto Nyoni ,Aidan Michael ,Hussein Said, Frank Domayo, Salum Abubaker ,Samata Mbwana ,Ngassa Mwrisho ('73 Athuman Idd),Thomas Ulimwengu, Kiemba Ramadhan.

Somalian referee, Wish Yabarow to officiate the game assisted by Kinde Musse (Ethipia), 1st assistant, Idam Mohamed (Sudan)-second assistant, Louis Hakizimana (Rwanda)-Fourth official, Richard Gahonzire (Rwanda)-Match commissioner and Referees' Inspector is Bernard Mfibusa (Burundi)

No comments:

Post a Comment