KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 7, 2013

Kilimanjaro Stars kukutana na wenyeji Kenya katika nusu fainali wa chalenji.

Mlinzi wa Azam fc ya jijini Dar es Salaam Jockins Atudo kwa mara nyingine amethibitisha ubora wake wa kuwa kikosini Harambee Stars ya Kenya baada ya kufunga bao muhimu kupitia mkwaju wa penati na kuipeleka timu yake katika nusu fainali ya michuano ya Chalenji.

Atudo, mfungaji wa bao pekee dhidi ya Rwanda amefikisha mabao matatu katika viwanja vitatu tofauti ambavyo Kenya walikuwa wakitumia kuanzia hatua ya makundi.

Amefunga mabao hayo katika uwanja wa Nyayo, Nakuru na leo Mombasa Stadia.

Sasa Kenya watakutana dhidi ya Kilimanjaro Stars ambao wamewaondosha mashindanoni mabingwa mara 13 Uganda kwa mikwaju ya penati.

No comments:

Post a Comment