Totternham imejiunga katika harakati za kunasa saini ya Edin Dzeko wakiwa na lengo la kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City hivi sasa yuko katika kipindi cha kuelelea kuumaliza msimu akiwa Etihad Stadium kabla ya kufanya maamuzi ya mwelekeo mpya.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City hivi sasa yuko katika kipindi cha kuelelea kuumaliza msimu akiwa Etihad Stadium kabla ya kufanya maamuzi ya mwelekeo mpya.
Spurs imeonyesha nia kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Bosnia ambaye pia anafukuziwa na vilabu viwili vya Inter na Napoli.
Dzeko ni miongoni mwa washambuliaji wa City pamoja na Sergio Aguero na Alvaro Negredo ambapo ameshafunga jumla ya magoli saba katika michezo 11 aliyoanza kuitumikia klabu hiyo msimu huu.
Dzeko ni miongoni mwa washambuliaji wa City pamoja na Sergio Aguero na Alvaro Negredo ambapo ameshafunga jumla ya magoli saba katika michezo 11 aliyoanza kuitumikia klabu hiyo msimu huu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akielezea kuumizwa kwake na kukosa nafasi ya kudumu ya kuanza licha ya kwamba hana msukumo wa maamuzi ya kuhama mwezi januari ambapo pia klabu ya City ina onekana haina nia ya kumruhusu aondoke kwa mkopo.
Dzeko atakuwa bado ana mwaka ndani ya mkataba wake mpaka kufikia kiangazi lakini atakuwa katika nafasi ya kuanza mazungumzo ya kuweza kuondoka kwa cut-price.
No comments:
Post a Comment