Meneja wa Manchester United David Moyes amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Robin Van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mweiz mmoja kutokana na matatizo ya nyama za mguu.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ataikosa michezo minne kutokana na tatizo hilo kabla ya kurejea tena uwanjani .
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ataikosa michezo minne kutokana na tatizo hilo kabla ya kurejea tena uwanjani .
Van Persie alikuwepo kwenye wa michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk,
akiingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Phil Jones na aliiumia wakati wa kuwania mpira wa kona.
Majeruhi hayo sasa yataifanya mabingwa hao watetezi wa Premier League watamkosa top scorer huyo katika kipinchi chote cha sikukuu za Christmas licha ya kwamba United haitakuwa na ratiba ya kucheza na timu yoyote iliyo katika nafasi kumi za juu mpaka watakapo kabiliana na Tottenham Old Trafford January mosi.
Moyes atamkosa mshambuliaji huyo Jumapili dhidi ya Aston Villa, ambapo atakuwa anataraji kurejea katika mwendo wa ushindi na kumaliza mzimu wa kutokushinda kwa michezo minn mfululizo katika ligi.
Moyes atamkosa mshambuliaji huyo Jumapili dhidi ya Aston Villa, ambapo atakuwa anataraji kurejea katika mwendo wa ushindi na kumaliza mzimu wa kutokushinda kwa michezo minn mfululizo katika ligi.
No comments:
Post a Comment