KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 12, 2013

Cristiano Ronaldo mshambuliaji bora wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa Ulaya

  Cristiano Ronaldo amepigiwa kura nyingi za mchezaji bora wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi kupitia mtandao wa Goal.com.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amevunja rekodi ya ufungaji ya mashindano hayo ya magoli tisa katika michezo mitano ya michuano hiyo akiwa na los Blancos ambapo ameweza kuisadia kutinga hatua ya mtoani pia akitoa pasi za mwisho za magoli mawili.

Ronaldo ameibuka mshindi kupitia kura za mtandao wa Goal ambazo zilianza Jumatano akipata asilimia 62.31 ya kura.

Zlatan Ibrahimovic akipata asilimia 16.9 na kushika nafasi ya pili kufuatia kufunga magoli nane katika kundi C akiwa na klabu yake ya Paris Saint-Germain magoli manne dhidi ya Anderlecht mwezi Oktoba.

Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey amepata asilimia 7.6 ya kura baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Olympique de Marseille na Borussia Dortmund na kuisaidia Gunners kutinga hatua ya mtoano.

Nafasi ya nne imekwenda kwa nyota wa Basel Mohamed Salah aliyepata asilimia 5.8 ambaye alifunga magoli mawili ya ushindi dhidi ya Chelsea na kuanza kutupiwa macho na watu wengu juu ya uwezo wake akiichezea mabingwa wa Uswiz ambao wamemaliza nafasi ya tatu baada ya matokeo ya kichapo dhidi ya Schalke.
Winga wa Bayern Munich Arjen Robben ameshika nafasi ya tano akifunga magoli matatu na pasi za kuzaa magoli mbili katika michezo minne tu kutokana na kukabiliwa na majeruhi, lakini hiyo imetosha kumpa asilimia 4.6.

No comments:

Post a Comment