KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 1, 2014

Dirisha lafunguliwa:Hatimaye Chelsea imekamisha usajili wa nyota wa Bertrand Traole aliyewafungia magoli Pre-season barani Asia.

 Chelsea imekamilisha usajili wa Bertrand Traole kwa mkataba wa miaka minne na nusu ambapo kiungo huyo wa kimataifa wa Birkina Faso ametabaisha kuwa kwake kufanikisha zoezi hilo ni sana na ndoto zake zimekuwa kweli.

Chelsea kutoka pande za London ya kaskazini kimsingi ilikuwa na mpango huo wa Traole mwenye umri wa miaka 18 tangu mwezi Oktoba na mpango mzima kukamilishwa hii siku ya mwaka mpya baada ya dirisha dogo rasmi kufunguliwa.

Traore alijiunga na kikosi cha Jose Mourinho kwa majaribio na kisha kuingia katika kikosi cha kwanza wakati wa ziara ya matayarisho ya kuanza msimu barani Asia ambapo alifanikiwa kuifungia Chelsea goli katika michezo miwili dhidi ya Malaysia XI na Indonesia All Stars.

Kinda huyo amefurahishwa na kusaini kwake ndani ya Stamford Bridge na amekuwa na ndoto kubwa ya kufuata nyayo za Didier Drogba .

"Nimefurahi sana, imekuwa ni uzoefu mkubwa kwa wachezaji wote wakubwa na nimejifunza mengi kutoka kwao" 

No comments:

Post a Comment