KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 1, 2014

Manchester City inakaribia kumsajili mchezaji wa under 17 wa Nigeria.

 Manchester City inakaribia kumsajili kiungo mchanga wa Nigeria mwenye umri wa miaka 17 Chidi Nwakali.

Nwakali, ambaye alikuwa vizuri katika kikosi cha Nigeria cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 mwezi Novemba, anatarajiwa kusafiri kuelekea Manchester akitokea Lagos akiwa na wazazi wake kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa City hapo kesho Januari 2.

Endapo mpango huo utafikiwa, Nwakali atakuwa akilipwa pauni £300,000 kwa mwaka ambapo ada ya uhamisho na stahili nyingine zitaanza kulipwa mpaka pale kiungo huyo atakapofikia umri wa miaka 18 Disemba 26 mwaka huu.

Nwakali pia anaweza kucheza kama mlinzi na kwasasa yuko katika Academy maarufu nchini Nigeria inayotambuliaka kama Shuttle Sports Academy ya jijini Lagos.

Mpango huu unakuja baada ya mpango wa awali wa kutaka kumsajili mchezaji mwingine wa Nigeria mwenye umri huo Kelechi Iheanacho, ambaye kimsingi ana makubaliano ya mdomo na Porto ya Ureno.

Iheanacho alikuwa katika kikosi kimoja na Nwakali katika kikosi cha Under-17 cha Nigeria katika fainali za kombe la dunia kwa vijana na alimaliza akiwa mfungaji bora kwa kufunga jumla ya mabao 6.

No comments:

Post a Comment