 |
Happy New Year! Cristiano Ronaldo akipiga pozi na mpenzi wake Inina Shayk, na rafiki Santa Claus kuukaribisha mwaka 2014. |
Wachezaji soka maarufu duniani wameingia katika mwaka mpya kwa mtindo tofauti huku wengi wengi wao wakiutumia mtandao wa Instagram kutupia picha mbalimbali walizopiga wakati wakiukaribisha mwaka mpya.
Kwa upande wake Gareth Bale mwaka uliopita ulikuwa ni mafanikio kwake kwani amefanikiwa kuvunja rekodi ya uhamisho kutoka katika klabu ya Tottenham na kujiunga na Real
Madrid kwa uhamisho uliokuwa na thamani ya pauni milioni £86.
Na jana usiku kuamkiia leo ulikuwa ni usiku mkubwa kwake akionekana katika picha akipozi na marafiki.
Nyota wa Real Madrid Gareth Bale akiwa katika picha na marafiki wakiukaribisha mwaka 2014
Cristiano Ronaldo alionekana akifurahia kwa kuweka picha akiwa na mpenzi wake Irina Shayk, na warembo wengine akiwemo Santa Claus.
Kwake nyota huyo wa Real Madrid alikuwa na mwaka mzuri uliopita na alistahili kushangilia kwani alifunga jumla ya mabao 69 katika jumla ya mechi 59 mwaka mzima uliopita.
Licha ya wapinzani wao wakubwa Barcelona kuwa katika kipindi kizuri cha kutwaa taji la ligi ya soka nchini Hispania La Liga Ronaldo anaaangaliwa kama mshambuliaji aliyeipeleka Ureno katika kombe la dunia akifunga mabao yaliyo iwezesha kuishinda Sweden katika michezo ya 'play-offs'.
Kwa upande wake Lionel Messi shujaa huyo wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina sherehe za mwaka mpya zilikuwa ni za kufana sana ambapo aliiutumia usiku wa jana kuukaribisha mwaka mpya kwa kugonga glasi ya shampeni na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wakati kengele za kuukaribisha mwaka zikisikika.
Licha ya kukabiliwa na majeraha na kuufanya mwaka kwenda hovyo,
Messi pia alikuwa na mazuri kadhaa kwani aliongeza tuzo ya ushindi wa La Liga msimu wa 2012-2013 akifunga pia magoli 56 katika jumla ya mechi 47 kwa timu yake na timu ya taifa.
Here's to you, Leo: Messi and partner Antonella share a glass of champagne at midnight
Mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski alitupia picha katika Facebook akiwa na rocket kubwa
Fernando Torres aliposti icha katika Instagram akiwa na mkewe
Good times: Nyota wa Barcelona Cesc Fabregas alitoka na marafiki zake
No comments:
Post a Comment