Ole Gunnar Solskjaer sasa ni dhahiri shahiri anaelekea kuwa meneja mpya wa klabu ya Cardiff City baada ya hii leo kuonekana uwanjani akiwa karibu na mmilikiwa klabu hiyo Vincent Tan katika mchezo dhidi ya Arsenal.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Norwey na klabu ya Manchester United kwasasa yuko kibaruani katika klabu ya The Molde ya huko Norwey ameonekana akiongozana na mmiliki wa Cardiff Tan kabla ya mchezo kuanza katika dimba la Emirates.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mancheseter United atayari anaonekana kama ni mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya meneja aliyetimuliwa Malky Mackay, ambaye alifutwa kazi na Tan mwezi Disemba.
Bosi wa muda David Kerslake amekuwepo katika benchi la ufundi katika mchezo wa leo pamoja na mchezo uliopita baina ya Cardiff dhidi ya Sunderland uliomalizika kwa sare ya 2-2 Jumamosi iliyopita.

Solskjaer leo alikuwa jukwaani ikiwa ni ishara ya kupewa kibarua rasmi..
Baada ya kuitumikia Old Trafford kwa mafanikio makubwa Ole Gunner Solskjaer ambaye kwasasa ana umri wa miaka 40 alielekea katika kazi ya ukocha na klabu yake ya kwanza ni FC Molde.
Aliingia katika kazi hiyo mwaka 2011 na kukiongoza kikosi hicho mpaka kuchukua taji la ligi ya Norwey .

No comments:
Post a Comment