Mshambuliaji wa Totternham Roberto Soldado ametaka timu yao icheze mchezo wa kushambulia wakati wote watakapokuwa wakikabiliana na mashetani wekundu Manchester United hii ikiwa ni siku ya mwaka mpya katika dimba la Old Trafford.
Timu hizo zinaingia katika mchezo wao wakiwa na alama sawa 34 kila moja huku vijana wa David Moyes wakiwa na kumbukumbu ya kumaliza ukame wa ushindi ndani ya Old Trafford dhidi ya Totternham msimu uliopita katika kipindi cha miaka 26 kwa ushindi wa mabao 3-2.
Soldado, ambaye alifunga goli katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-0 amekuwa akiutamani mchezo huo na anadhani kikosi chao kitaibuka na ushindi tena endapo kama wataingia katika njia ya kweli.
Pia nyota huyo wa kimataifa wa Hispania hakusita kumsifia mshambuliaji mwenzake Emmanuel Adebayor, ambaye amekuwa katika kiwango bora tangu aliporejea katika kikosi cha kwanza cha kocha Sherwood.
No comments:
Post a Comment