STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 01 Januari, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amewataka wananchi kujenga na kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi
ili kuimarisha afya zao pamoja na kujikinga na maradhi yanayoweza
kuepukika.
Dk.
Shein ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa akizungumza na wanachama
wa klabu za mazoezi na vyama vya michezo katika Bonanza Maalum la
Mazoezi ya Viungo lililofanyika katika uwanja wa Amaan mjini Unguja.
Kabla
ya kuzungumza na wanamichezo hao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi akiwa amefuatana na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim
Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi pamoja na
viongozi wengine walioshiriki matembezi ikiwa ni sehemu ya Bonanza hilo
yaliyoanzia Michenzani mjini Unguja hadi Uwanjani hapo.
Dk.
Shein aliwaeleza washiriki kuwa ni jambo lililo dhahiri kuwa kufanya
mazoezi ni jambo la msingi sana katika kuimarisha afya ya mwili na
kuchangamsha akili hivyo Serikali ina kila sababu ya kuziunga mkono
jitihada walizozianzisha za kuunda vikundi vya mazoezi.
Alifafanua
kuwa hivi sasa kumekuwepo na maradhi mengi ambayo hapa kwetu yanaelezwa
kusababishwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha na kuyataja maradhi hayo
kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari na kuongezeka unene
ambayo yanaweza kupunguza kwa kufanya mazoezi.
Pichani chini Dr Shein akiongoza matembezi ya Bonanza la vikundi vya mazoezi ya viungo
Kikundi cha Brassband cha Mafunzo kikiwa mbele ya
Matembezi ya Bonanza la 5 la Vikundi vya Mazoezi ya
Viungo,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi mbali mbali
wakishiriki,matembezi hayo yameanzia Uwanja wa Kisonge,hadi uwanja wa
Amaan Wilaya ya Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohamed Shein,(katikati) na viongozi mbali mbali
walioshiriki,Matembezi ya Bonanza la 5 la Vikundi vya Mazoezi ya
Viungo, yaliyoanzia Uwanja wa Kisonge,hadi uwanja wa Amaan Wilaya ya
Mjini Unguja,
Wanavikundi vya mazoezi ya Viungo wa Zone A,wakiwa
katika Matembezi ya Bonanza la 5,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi
mbali mbali wakishiriki,matembezi hayo yaliyoanzia Uwanja wa
Kisonge,na kumalizia Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja
Kikundi cha Mazizini Beach Exercise Group,hawakuwa
nyuma katika Matembezi ya Bonanza la 5,yanayoongozwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein,na viongozi mbali mbali wakishiriki,matembezi hayo yaliyoanzia
Uwanja wa Kisonge,na kumalizia Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini
Unguja
Kikundi cha Training & Fitness Obama Club,wakiwa
katika Matembezi ya Bonanza la 5,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi
mbali mbali wakishiriki,matembezi hayo yaliyoanzia Uwanja wa
Kisonge,na kumalizia Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja
Kikundi cha Mchezo wa Judo,wakiwa katika Matembezi ya
Bonanza la 5,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi mbali mbali
wakishiriki,matembezi hayo yaliyoanzia Uwanja wa Kisonge,na kumalizia
Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja
No comments:
Post a Comment