Baada ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Ernie Brandts, klabu ya Yanga imelimaliza benchi lote la ufundi kwa kulifuta kazi ambapo hii leo imewakabidhi rasmi aliyekuwa kocha msaidizi mlinzi wa pembeni wa klabu hiyo Freddy Felix Minziro na aliyekuwa kocha wa makipa raia wa Kenya Razaki Siwa.
Taarifa za hivi punde zimeaarifu kuwa makocha hao wamefutwa kazi kutokana na sababu zilezile zilizomfuta kazi Ernie Brandts na kwamba kwasasa uongozi wa klabi hiyo inakamilisha mipango ya kupata kocha mkuu mpya huku kocha wa zamani wa AFC Leopard ya Kenya Luc Eymael akitajwa kuwa ni miongoni mwa makocha wanatupiwa macho na mabingwa hao wa soka Tanzania bara.
Tayari Yanga imeshakwisha muajiri kocha Charles Bonface Mkwasa ambaye pia ni kiungo wa zamani wa klabu hiyo, ambaye amepewa jukumu la Minziro la kuwa kocha msaidizi. Kabla ya uteuzi wake Bonface alikuwa kocha mkuu wa Ruvu Shooting ya Pwani.
No comments:
Post a Comment