- Liverpool, Arsenal na Tottenham wote wako mbioni kumnasa Alvaro Morata
- Barcelona ikiwa katika mawindo ya Nemanja Vidic kuziba pengo la Carles Puyol
- West Ham inakaribia kumalizia saini ya Lacina Traore kwa mkopo
- Tom Ince ananusa kuelekea Swansea au Palace ama kusalia Blackpool
- Manchester United, City na Chelsea wanamsaka Eliaquim Mangala
- Aiden McGeady kujiunga na Everton kiangazi.
Liverpool ndio klabu ya hivi iliyopewa nafasi kubwa ya kumsajili Alvaro Morata.
Meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers amekuwa akihaha kumsajili mshambuliaji huyo na pia kumekuwepo na habari nyingine zikiarifu kuwa nyota huyo wa kimataifa wa kikosi cha Under 21 cha Hispania Morata amekuwa katika mpango wa kibiashara katika vilabu vya Arsenal, Tottenham na Inter Milan .
Carlo Ancelotti amekuwa hafurahishwi na kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 ambapo hana uwezo wa kukabiliana na akina Karim Benzema na nguvu kama Jese, hivyo mpango wake ni kumruhusu aende kokote kwa mkopo.
Wanataka ada ya karibu pauni milioni £1.5 lakini anataka kupewa uhakika kama mshambuliaji huyo atapata nafasi ya kucheza.
Liverpool huenda ikashindwa kufanya hivyo kwakuwa tayari Rodgers anaonekana kuanza kupendelea kuwatumia zaidi Daniel Sturridge acheze pacha na Luis Suarez lakini pia meneja huyo anaonekana kuwa katika mpango wa kumrejesha Victor Moses kutoka Chelsea kutokana na kutokuvutiwa na mkopo wake huku pia anaonekana hajaanza kufikiria juu ya mpango mwingine wa uhamisho utakao muhusu Iago Aspas.
Rodgers bado yuko sokoni akisaka bidhaa hususani Mohamed Salah wa Basle lakini inavyoonekana klabu hiyo ya Uswiss imemthaminisha kwa kiwango cha juu sana tofauti na Liverpool ilivyo dhani huku vilabu vingine vya Bayer Leverkusen, Inter Milan na Atletico Madrid wakionekana kuvutiwa na mshambuliaji huyo raia wa Misri.
Mlinzi wa kushoto pia ni mpango wa Liverpool ambapo Aly Cissokho akionekana kushindwa kuwavutia tangu alipojiunga nao akitokea katika klabu ya Valencia.
Pia, Liverpool inakabiliwa na upinzani kutoka katika klabu ya Roma juu ya usajili wa Martin Montoya wa Barcelona.
Mlinzi huyo wa pembeni mwenye uwezo mkubwa 'Versatile' anategemewa kuwa nje ya makataba wakati wa kiangazi lakini anaonekana kufurahia zaidi uwepo wake ndani ya Barca na akisubiri ofa nyingine ya klabu yake.
Wednesday, January 8, 2014
Liverpool yaungana na Arsenal na Spurs katika mbio za kusajili Morata, Barca inamkufuzia Vidic huku Traore ajipianga kuelekea kwa mkopo West Ham
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment