Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic atakosa mechi ya
nusufainali ya marudiano katika League Cup dhidi ya Sunderland uwanjani
Old Trafford Jumatano baada ya kushindwa kubatilisha kadi nyekundu
aliyopowa wikendi iliyopita.
Mlinzi huyo wa kati mwenye shughuli kubwa aliwasilisha malalamishi ya kutolewa uwanjani
bila hatia baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu wakati wa mechi ya Ligi
ya kuu ambapo mabingwa United walilazwa 3-1 na Chelsea uwanjani
Stamford Bridge Jumapili. Vidic alidaiwa kumchezea visivyo Eden Hazard.
Vidic alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja, ambayo kawaida huandamana na marufuku ya kutocheza mechi tatu.
Tume huru ya kinidhamu ilithibitisha jana Jumanne kwamba marufuku hiyo
itatekelezwa “mara moja”, kuanzia mechi ya leo Jumatano ambapo United
wanajaribu kupindua matokeo ya kufungwa mabao 2-1 walikopokezwa mechi ya mkondo wa
kwanza.
"Malalamishi ya Nemanja Vidic wa Manchester United kwamba alifukuzwa
uwanjani kimakosa yamekataliwa na tume huru ya kinidhamu,” ilisema
taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Uingereza Jumanne.
"Kwa hivyo, marufuku ya mechi tatu kwa mchezaji huyo inaanza
kutekelezwa mara moja. Vidic alionyesha kadi nyekundu kwa kucheza vibaya
wakati wa mechi ya timu yake dhidi ya Chelsea Jumapili 19 Januari
2014.”
Mserbia huyo wa miaka 32 pia atakosa mechi za United katika ligi dhidi ya Cardiff City nyumbani na ugenini dhidi ya Stoke City.
United walizoea kutojishughulisha sana na League Cup chini ya meneja
wa zamani Alex Ferguson, ingawa walishinda kikombe hicho mara nne chini
ya raia huyo wa Scotland na badala yake walisaka vikombe vya hadhi
zaidi.
Lakini kufuatia kichapo cha Jumapili ambacho kimeacha timu hiyo ya
David Moyes alama 14 nyuma ya viongozi wa Ligi ya Premia Arsenal, na
baada ya kubanduliwa Kombe la FA na Swansea City, United wanahitaji
sana ufanisi katika League Cup.
No comments:
Post a Comment