KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 22, 2014

Southampton yamtangaza mkuu wake wa fedha kushika nafasi ya mwenyekiti kwa muda

Southampton imemtaja afisa mkuu wa masuala ya kifedha Gareth Rogers kushika nafasi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo kwa muda mpaka kumalizika kwa msimu. 

Mbadiliko hayo yanafanyika ili kumpa nafasi mmiliki wa klabu hiyo Katharina Liebherr muda zaidi wa kusaka mrithi wa kudumu nafasi ya mwenyekiti ambayo iliachwa wazi na Nicola Cortese, ambaye aliondoka mapema mwezi huu.

Liebherr alifanya mazingumzo na mwenyekiti wa zamani wa Blackburn John Williams wiki iliyopita na amesalia kuwa mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo kwa minajili ya kudumu.

Hali ya mambo ilivyokuwa ndani ya klabu hiyo

2009 - Marehemu baba yake na Katharina Liebherr, Markus, alitoa kiasi cha pauni milioni £14 kuokoa klabu hiyo katika mambo ya utawala kupitia kampuni yake ya Mali Holdings.

2010 - Baada ya baba yake kufariki dunia mwezi Agosti 2010, Katharina Liebherr akarithi kampuni ya Mali Holdings.

2013 - Mwezi Oktoba, Liebherr aliteuliwa na bodi kuwa mwenyekiti.
 
2013 - tarehe kama hiyo Nicola Cortese akaandika barua ya kujiuzulu katika nafasi ya mwenyekiti.

2014 - Cortese akaondoka katika klabu, na kumfanya Liebherr kutokuwa mtendaji wa juu wa klabu hiyo 'non-executive chairman'.

Liebherr anakaririwa akisema
"Ninayofuraha kuwa Gareth amekubali kushikilia nafasi hii."

Rogers, meneja wa juu wa zamani katika kampuni ya mahesabu ya Deloitte, amekuwepo Southampton tangu Machi 2011. 

No comments:

Post a Comment