KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 22, 2014

Manchester City wanasubiri jibu la jeraha la bega la Alvaro Negredo

Manchester City italazimika kusubiri kwa muda kujua ukubwa wa maumivu ya mshambuliaji wao Alvaro Negredo ambaye akutana na dhahma ya maumivu ya bega.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 28, alipatwa na maumivu hayo katika dakika za mwisho za mchezo wa michuano ya Capital One hatua ya nusu fainali ambao City waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham United licha ya kuamliza mchezo huo.

Amekaririwa meneja wa City Manuel Pellegrini akisema
"Ana maumivu kwa sasa na tunasubiri kujua kama ni makali au laa" .
Klabu hiyo imethibtisha kuwa hilo litafahamika hapo kesho Alhamisi baada ya uchunguzi kufanywa.

Negredo alifunga magoli mawili katika mchezo huo uliopigwa ikiwa ni magoli mengine ya ziada baada ya kufunga magoli matatu yaani hat-trick katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali.
Mshambuliaji huyo alijiunga na City akitokea Sevilla kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £20 Julai mwaka jana na amekuwa muhimu Etihad.
Amefunga jumla ya magoli 23 katika jumla ya michezo 33 ya michuano yote na amekuwa akifananishwa na wakali wa zamani kama ilivyokuwa kwa Alan Shearer kabla ya kustaafu mwaka 2006.
Kwasasa ana magoli tisa katika jumla ya michezo sita ya michezo iliyopita.

No comments:

Post a Comment