Manchester United imeweka mezani mpango wa pauni milioni £35 kwa ajili ya kiungo wa Chelsea Juan Mata.
Mata mwenye umri wa miaka 25, amehusishwa na kuelekea Stamford
Bridge baada ya kuonekana akiwa katika hali ngumu ya kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya Jose
Mourinho.
United imekanusha kuweka mpango huo rasmi lakini mpango wa awali unaonekana kufanyika kupitia mtu wa kati kwa niaba ya klabu hiyo ambao ni mabingwa wa Premier League.
Mata hajafanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Chelsea hii leo.
Jana, Chelsea ilisisitiza kuwa that Mata, ambaye alipigiwa kura kuwa mchezaji wa mwaka wa klabu yake kwa miaka miwili mfululizo hayuko sokoni.
Hata hivyo kiungo huyo ambaye ni sehemu ya kikosi cha Hispania kilichoshinda kombe la dunia mwaka 2010 na 'European Championship' mwaka 2012, amekuwa akibadilishwa katika michezo tisa kati ya michezo 13 ya ligi kuu ya Premier msimu huu hali ambayo imekuwa ikiongeza nguvu tetesi za klabu ya Manchester United kuweka mpango wa kumsajili katika dirisha la usajili.
No comments:
Post a Comment