Shiriksho la mchezo wa soka duniani FIFA, limetoa
onyo kwa utawala nchini Brazil, kuwa mji wa kusini wa Curitiba huenda
ukaondolewa miongoni mwa miji itakayoandaa fainali ya kombe la dunia,
kutokana na kuchelewesha kwa shughuli za ujenzi.
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema kuwa ukarabati katika uwanja huo unaendelea kwa mwendo wa pole sana.
Ametaja suala hilo kama la muhimu na kuwa FIFA
itatangaza katika kipindi cha mwezi mmoja ujao ikiwa mji huo wa Curitiba
utasalia kama moja ya miji itakayokuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Huku ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla
ya fainali hizo kuanza viwanja sita kati ya kumi na mbili
vinavyohitajika vimekamilika.
No comments:
Post a Comment